Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Ajib: Akili ilitaka, mwili ukatenda

Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib amesema bao alilofunga lilitokana na akili yake kutulia na kufanya uamuzi sahihi. Ajib alifunga ...



Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib amesema bao alilofunga lilitokana na akili yake kutulia na kufanya uamuzi sahihi.
Ajib alifunga bao katika dakika za mwisho za mchezo huo wakati Yanga ikichapa Mbao fc kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ajib alipiga tiktak na mpira kwenda moja kwa moja wavuni na kumfanya kipa wa Mbao auangalie tu mpira huo.
Ajib amesema wakati mpira ulivyofika kwake aliona ni wakati sahihi kufunga akiwa eneo hilo na akili yake ikamwambia afunge kwa staili hiyo.
Amesema amewahi kufunga bao kama hilo miaka ya nyuma na sasa anazidi kumuomba Mungu awe na mwendelezo mzuri wa kiwango chake.
Akizungumzia kutoitwa Taifa Stars, Ajib amesema bado hajakata tamaa akiamini kwamba nafasi yake kurudi kulitumikia taifa bado ipo ataendelea kujituma ili kurudisha nafasi yake.
Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, alisema bao ambalo amefunga mchezaji wake ni zuri na anatagemea kuliona kuwa la msimu.
"Pongezi iende kwa timu nzima, lakini Gadiel amekuwa vizuri katika kupiga pasi za mwisho, alikimbia vizuri na kupiga krosi ambayo ilizaa bao, nazani hili linaweza kuwa goli la msimu," alisema.
Akizungumzia kuhusu wachezaji wake wawili waliopo timu ya Taifa na kuumia katika pambano hilo (Beno na Andrew) alisema inawezekana kutokana na kuchanganya programu mbili tofauti.
"Sitaki kuongelea hayo mambo kwa undani zaidi lakini kila mmoja kaona wachezaji walioumia katika mchezo huu wote walikuwa timu ya Taifa, nazani misuli ilikuwa ikiwasumbua," alisema Mwandila.
Aliongeza kwamba kukosekana kwa Papy Tshishimbi katika mchezo huo  ni baada ya kupata majeraha ya enka kwenye mazoezi ya mwisho.

No comments