Kwa miaka mingi tuu mawasiliano kwa njia ya simu za mikononi yamerahisishwa na kuwa ya gharama nafuu sana tangu kutokana na uwezo wa kuji...
Kwa miaka mingi tuu mawasiliano kwa njia ya simu za mikononi yamerahisishwa na kuwa ya gharama nafuu sana tangu kutokana na uwezo wa kujiunga kifurushi/vifurushi kwenye mtandao wa simu husika.
Ushindani kwenye makampuni ya simu upo kila uchwao kwa kila mhusika kujaribu kuja na kitu kizuri kuvutia wateja wake na hata kupata wateja wapya. Halotel yenye miaka karibu minne (4) tangu ianze kutoa huduma za mawaasiliano nchini Tanzania imekuwa ikionekana kukua mwaka hadi mwaka na hii kwa maoni yangu inatokana na kuwa na miundombinu ya mawasiliano mizuri mijini mpaka vijijini lakini pia hata kuwa na vifurushi murua kabisa.
Halotel Tanzania wameongeza vifurushi viwili vilivyozinduliwa mnamo Februari, 19 2019 viitwavyo “Royal Bando” na “Tomato Bando“. Sasa undani wa vifurushi hivyo ndio unavutia mbali na majina yenyewe:Royal Bando ni kifurushi ambacho kinalenga zaidi gharama nafuu za kupiga simu za kimataifa (India, Uchina, Canada na Marekani) lakini mbali na hapo mteja atayenununua kifurushi hicho atapata pia dakika, MB na SMS. Kifurushi hiki chenye kauli mbiu “Ishi kifalme” kipo katika makundi manne; Tsh. 10,000, 20,000, 30,000 na 50,000 kwa mwezi mmoja.Kwa kifurushi cha ROYAL Tsh. 10,000 mteja atapata dakika 120 za kupiga mtandao yote (ndani na nje), dakika 300 Halotel-Halotel, SMS 500 na 2GB za intaneti kwa kasi isiyokuwa na ukomo.AUMteja anaweza akanunua kifurushi hicho hicho na kupata dakika 200 kupiga mitandao yote (ndani na nje), SMS 500 na 0.5GB za intaneti kwa kasi isiyokuwa na ukomo.Tomato Bando ni kifurushi ambacho kinapatikana kwa gharama ya Tsh. 1,000, 3,000 na 5,000 lakini ili mteja aweze kufurahia huduma hii inapaswa awe na laini ya Halotel-Tomato ambayo atainunua kwa Tsh. 8,000 tu.Laini hiyo itamuwezesha kupiga simu kwa kila namba yoyote ya Halotel bure kwa dakika 5 za mwanzo. Licha ya hilo mteja atapata salio la ziada la Tsh. 4,000 BURE ambalo atalitumia kwenye huduma nyingine anazopenda kutoka Halotel. Ili kuweza kujua salio hilo la ziada, mteja atapiga *102#.
No comments