Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Samsung Galaxy Fold: Simu ya kwanza ya display/kioo cha mkunjo

Samsung Galaxy Fold: Kutoka Simu kwenda Tableti… Wengi walitegemea Samsung wangeonesha tuu simu hii na kusema itatoka mwishoni mwa mwak...


Samsung Galaxy Fold
Samsung Galaxy Fold: Kutoka Simu kwenda Tableti…

Wengi walitegemea Samsung wangeonesha tuu simu hii na kusema itatoka mwishoni mwa mwaka au ata mwakani, ila Samsung wametambulisha na kusema itaanza kupatikana ndani ya miezi miwili kuanzia sasa – yaani Samsung Galaxy Fold itapatikana Aprili

Samsung wamekuwa na lengo la kuleta simu hii kwa muda sasa, na miezi michache iliyopita Xiaomi walionesha ya kwao na kukawa na uwezekano wa wao kuwapiku Samsung kwa kuwa wa kwanza kuleta simu ya namna hii sokoni ila kumbe Samsung wapo mbele zaidi – simu ipo tayari kuingia sokoni.

Je Samsung Galaxy Fold ni simu ya namna gani?

Kama jina lake lilivyo, ‘fold’ ni kimombo cha kukunja/mkunjo, Galaxy Fold ndio jina waliloipa simu yao yenye uwezo wa kutumika kama simu na kisha pia kuweza kufunguliwa na kupata uso mpana zaidi na kuwa tabelti.
samsung galaxy fold
Muonekano ikiwa inatumika kama tableti, na ikiwa inatumika kama simu ya kawaida
Simu ya Galaxy Fold ikiwa imekunjwa inakioo/display kidogo mbele ambacho unaweza kutumia kama simu ya kawaida wakati Galaxy Fold ikiwa katika umbo dogo – la inchi 4.6.
Pale utakapotaka kuitumia kama tableti basi utaifungua na ndani ya sekunde moja app yeyote uliyokuwa unaitumia wakati huo itajifungua kwa upana katika display/kioo cha ndani cha inchi 7.3 (sentimeta 18.5).

Ukubwa huu unaifanya katika umbo la tableti iwe na uwezo wa kufungua app tatu kwa wakati mmoja mbele ya mtumiaji kwenye display hii kubwa.
samsung galaxy fold
Samsung wamesema eneo la mkunjo wa simu hii linaweza kuhimili maelfu ya mikunjo na mifunguo
Kiungo chake kinachounganisha pande mbili Samsung wamesema wametumia teknolojia ya kisasa sana kuhakikisha kitadumu mara maelfu ya ufunguaji na ufungaji. Pande zote mbili zinahifadhi betri kuhakikisha kifaa hichi kinadumu na chaji muda mrefu – mAh 4,380.
Galaxy Fold
Utumiaji wa app tatu kwa wakati mmoja ndani ya Galaxy Fold
Galaxy Fold inamaeneo matatu yenye kamera – Nyuma kuna kamera tatu, ndani kwa ajili ya selfi kipindi unaitumia kama tableti kuna kamera mbili.. na wakati unaitumia kama simu kuna kamera moja ya selfi.

Sifa zingine; 
  • Inakuja na RAM ya GB 12,
  • prosesa ambayo Samsung hakuitaja – inaaminika itakuwa ni ya kwao na si Snapdragon.
  • Diski ujazo ni wa GB 512.
  • Inakuja na uwezo wa 4G na toleo la 5G lipo njiani.
Katika bidhaa ambazo Samsung wametambulisha hivi karibuni hii ndio bidhaa isiyo na uhakika sana wa hali ya soko. Ukiangalia bei yake ni kubwa sana na hili linaweza kuwafanya watu kuona ni rahisi zaidi kuwa na kununua tableti na simu kama vitu tofauti.

Toleo la 4G litaanza kupatikana mwezi wa 4 tarehe 26 kwa bei ya dola 1,980 (zaidi ya Tsh Milioni 4.6).

Vipi una mtazamo gani na Samsung Galaxy Fold?

No comments