WAKATI beki tegemeo wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani akishindwa kusaļ¬ ri na kikosi hicho kwenda Lindi kuwavaa Namungo FC, mshambuliaji Ami...
WAKATI beki tegemeo wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani akishindwa kusaļ¬ ri na kikosi hicho kwenda Lindi kuwavaa Namungo FC, mshambuliaji Amissi Tambwe amesema wataweka rekodi.
Yanga imesaļ¬ ri jana Alfajiri kuwafuata Namungo mkoani Lindi kwa ajili ya kucheza mechi ya Kombe la FA itakayopigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani humo.
Katika mchezo huo, Yanga wataingia uwanjani wakiwa na morali kubwa baada ya kutoka kuvunja mwiko kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa kuifunga Mbao FC mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu. Yondani hajasaļ¬ ri na kikosi cha Yanga kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano.
FOLLOW US
Zahera alisema, licha ya kukosekana beki huyo anafurahia kwani ana mabeki wengi wa kati huku akipanga kumtumia Andrew Vicent ‘Dante’ atakayechukua nafasi ya Yondani katika mchezo huu ambaye kwenye mchezo na Mbao alianzia benchi.
“Yondani tumemuacha Dar, hivyo hatakuwa katika sehemu ya kikosi changu nitakachokitumia katika mchezo huu dhidi ya Namungo ambao nimepanga kuwafunga ili tusonge mbele zaidi.”
Tambwe ambaye alifunga hat trick kwenye mchezo dhidi ya Tukuyu Stars alisema, wamepanga kuweka rekodi ambayo itawashangaza wengi.
“Rekodi yenyewe ambayo tumepanga kuiweka ni ya kuibuka na ushindi wa mabao mengi katika mchezo huo, ambao utatuwezesha kutinga robo fainali ya michuano hiyo.
“Tutaingia uwanjani kupambana kwa nguvu zote kama ambavyo tumekuwa tukifanya dhidi ya timu nyingine tulizokutana nazo kwa hiyo ni lazima tuandike rekodi katika mechi hiyo,” alisema Tambwe.
No comments