Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MTIBWA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA SIMBA

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa hesabu zoa kubwa ni kupata pointi tatu muhimu mbele ya Simba mchezo unaotarajiwa kuchez...


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa hesabu zoa kubwa ni kupata pointi tatu muhimu mbele ya Simba mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 17 uwanja wa Uhuru.

Mtibwa Sugar walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli FC itamenyana na Simba ambayo ilishinda mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania uwanja wa Uhuru.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao Simba ila wanachohitaji ni pointi tatu.

“Mchezo wa kwanza tulipoteza mbele ya Lipuli sasa ni muhimu kwetu kushinda mchezo wetu wa Simba tunahitaji kupata pointi tatu zao ili kujiweka kwenye mazingira ya ushindani.

“Kushindana na timu bora ni jadi yetu kwani nasi tuna kikosi bora chenye uwezo wa kupambana mashabiki watupe sapoti ya kutosha kupata burudani,” amesema Kifaru.

No comments