Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MVULANA KENYA ATUNUKIWA

Picha ya kijana mdogo akichunga ng'ombe akiwa amevaa jezi au fulana aliyoiandika jina la Mesut Ozil na chapa ya number ya mchezaji huy...


Picha ya kijana mdogo akichunga ng'ombe akiwa amevaa jezi au fulana aliyoiandika jina la Mesut Ozil na chapa ya number ya mchezaji huyo imewavutia wengi katika mitandao ya kijamii akiwemo nyota mwenyewe wa soka.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Mesut Ozil amemnyooshea mkono mvulana mdogo kutoka nchini Kenya, Lawrence ambaye picha yake akiwa amevaa jezi bandia ilitumwa katika ujumbe wa twitter kwenye akaunti ya Ozil mwaka jana.

Picha ya Lawrence akiwa amevaa jezi halisi iliyotiwa saini na nyota huyo, mojawapo kati ya tano alizotumiwa kama zawadi, imesambazwa katika mitandao ya kijamii na kupendwa na kupongezwa na wengi.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD

Akizungumza na BBC, Eric Njiru mwandishi nchini Kenya aliyempiga picha mvulana huyo mwaka jana, anasema anahisi furaha sana kwa kuwa amefanikiwa kumuunganisha mchezaji wa kimataifa, wa timu ya taifa Ujerumani, aliyeshinda kombe la dunia, na kijana ambaye anatoka maeneo ya Nairobi.

'Sio watu wengi wanaoweza kupata fursa ya kuongea na mchezaji wa Uingereza, wacha hata ligu ya juu, hata kwa ligi za chini, sisi wenyewe wakenya hatujapata fursa ya kuongea na mchezaji kama Origi ambaye babake ni Mkenya', amesema Njiru akielezea fursa hiyo adimu.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD


Ameeleza huenda Lawrence ni mdogo kwa sasa kutambua thamani ya fursa hiyo lakini anaamini akiwa mkubwa na akitazama nyuma, atatambua ukubwa wa hatua hiyo.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD

Njiru aliituma picha hiyo mwishoni mwa mwaka jana kama ujumbe kwenye akaunti ya twitter ya Ozil.

PAKUA APPLICATION YETU   CLICK TO DOWNLOAD

No comments