Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

SIMBA WAJIPANGE KUPINDUA MEZA

UNAAMBIWA wapinzani wa Simba, kwenye hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika,  AS Vita licha ya kuvujishiwa siri za Simba na kocha wa Yan...



UNAAMBIWA wapinzani wa Simba, kwenye hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika,  AS Vita licha ya kuvujishiwa siri za Simba na kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera wana uchu wa kucheza mpira wakiwa Uwanjani hivyo Simba wajipange kweli kesho kupindua meza.

 Simba kesho wanatakiwa wapate ushindi wa aina yoyote ili kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano hii.

Vita kubwa itakuwa kwa makocha wawili Patrick Aussems wa Simba na Ibenge wa Congo ambaye kwenye mchezo wa kwanza Simba waliangukia pua kwa kufungwa mabao 5-0 nchini Congo.

Kila mmoja anatafua nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali hivyo mwenye hesabu kali atashinda mchezo wa kesho.

AS Vita kutoka Congo iliyo chini ya kocha Florent Ibenge, ambaye ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Congo akiwa ni bosi mkubwa wa Zahera.

Kwenye mazoezi ya jana ambayo yalifanyika Viwanja vya Gymkkhana, wakiwa chini ya ulinzi mkali kwa kugoma waandishi wa habai kuingia, walifanya mazoezi kwa muda wa dakika 97 bila kuonyesha kuchoka jambo ambalo linamaanisha Simba wajipange kwa spidi ya hawa wacongo.

Licha ya jua kuwapiga, bado wacongo hao waliendelea kukazana kuiwinda Simba kwa kufanya mazoezi maalumu ambayo walipewa mipango mapema na kocha wao Ibenge kama ifuatavyo:-

Baada ya kufika Uwanja wa mazoezi, wachezaji waliingia kati ya Uwanja na kufanya sala ya pamoja huku mbeba mipira akiimwaga chini mipira yote ya wachezaji.

Baada ya kumaliza kusali waliifuata mipira na kuanza kujifunza kufanya mazoezi ya umiliki wa mpira ambapo walianza kwa spidi kali na kumaliza kwa spidi kali kuliko ile ya awali.

Pia walijigawa wachezaji nane nane ili kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe kwa kuanza nusu Uwanja kisha baadaye wakatumia Uwanja mzima kufanya mazoezi.

AS Vita walionyesha umakini katika kumiliki na kutoa pasi, kukaba kwa nguvu na akili jambo ambalo linapaswa litazamwe kwa ukaribu na wachezaji wa Simba.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kupiga pasi ndefu na fupi 
hii inaamanaisha kwamba AS Vita ni timu yenye spidi kali na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira Uwanjani kutokana na mazoezi ambayo wameyafanya jana na leo Uwanja wa Taifa hivyo wachezaji wa Simba wasitarajie wepesi.

Ikumbukwe kuwa kocha wa AS Vita anafanya kazi kwa ukaribu na kocha wa Yanga ambaye anaijua vizuri Simba na aliweka bayana kwamba hatakuwa mchoyo wa kumwambia bosi wake kama atahitaji kujua uzuri wa Simba na ubaya wa Simba

No comments