Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

'Hamisa akubali kuwa mke wa pili wa Diamond baada ya Zari'

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amesema kuwa alikuwa tayari kuwa mke wa pili wa Diamond Platnumz iwapo angemuoa Zari The Bosslady. Hamisa a...

'Hamisa akubali kuwa mke wa pili wa Diamond baada ya Zari'

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amesema kuwa alikuwa tayari kuwa mke wa pili wa Diamond Platnumz iwapo angemuoa Zari The Bosslady.

Hamisa akizungumza kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya, amesema hata angeolewa na akawa mke wa kwanza hawezi kumkataza mume wake kuoa mwanamke mwingine. 


Kauli ya Hamisa inakuja pindi alipoulizwa wakati anaanza mahusiano na Diamond hakumuuliza kuhusu Zari ambaye alikuwa mpenzi wa muimbaji huyo kwa wakati huo.

"Nilimuuliza akasema Muislam anaweza kuoa wanawake wengi, Yeah hata kama ikitokea nimeolewa mke wa kwanza, ikatokea anataka kuongeza mwanamke mwingine am ok with that, nilikuwa tu sawa kwa sababu ni kitu ambacho nimeshakipitia," amesema Hamisa.


Kwa sasa Hamisa Mobetto yupo nchini Kenya kwa ajili ya kufanya media tour ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Madam Hero.


No comments