Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MAKAMBOVIC AZIDI KUING'ARISHA YANGA

Timu ya Yanga imeendelea kujiwekea malengo mazuri ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ...


Timu ya Yanga imeendelea kujiwekea malengo mazuri ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Mchezo huo ulioshuhudiwa ukipigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ulizitikisa nyavu za wagosi wa kaya mnamo dakika ya 12 kupitia kwa Heritier Makambo 'Makambovic'.

Bai hilo limeisaidia Yanga kujikusanyia jumla ya alama 9 mpaka sasa ikishinda mechi zake zote tatu.

Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alimuanzisha kama kawaida kipa mkongomani Klaus Kindoki ambaye alipokea lawama kali katika mechi iliyopita.

Kindoki aliruhusu kufungwa mabao matatu matatu dhidi ya Stand United huku wakiibuka na ushindi wa mabao 4-3 lakini leo ameonekana kulitendea haki lango la timu yake

No comments