Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Mtangazaji Zamaradi kurejea kwenye TV Show kisa Irene Uwoya

Ni kipindi kirefu sasa Mtangazaji Zamaradi Mketema hajaonekana kwenye TV Show kitu kilichompa umaarufu mkubwa. Hata hivyo kuna uwezekano Z...

Mtangazaji Zamaradi kurejea kwenye TV Show kisa Irene Uwoya

Ni kipindi kirefu sasa Mtangazaji Zamaradi Mketema hajaonekana kwenye TV Show kitu kilichompa umaarufu mkubwa.

Hata hivyo kuna uwezekano Zamaradi akarejea tena kwenye kazi hiyo na hii ni kutokana na kuhitaji kufanya mahojiano na Irene Uwoya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; 


"Nahitaji interview moja kubwa sana na wewe, nina sababu kama milioni hivi... ntarudi kwenye Screen kwa ajili yako."

Utakumbuka Zamaradi alifanya vizuri zaidi alipokuwa akitangaza kipindi cha Take One kilichokuwa kikiruka kupitia Clouds TV. Kwenye kipindi hicho awali aliwahoji wasanii wa filamu na baadaye watu mbalimbali wenye nguvu ya ushawishi kwenye jamii kama wasanii wa Bongo Fleva, Watangazaji na wengineo.



No comments