Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MAAMUZI MAGUMU YA MOURINHO KWA POGBA HAYA HAPA

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa hana tatizo na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba licha ya kumwambia mchezaj...


Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa hana tatizo na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba licha ya kumwambia mchezaji huyo kwamba hatowahi tena kuwa nahodha wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa BBC, Mourinho alimwambia Pogba kwamba sio nahodha wa klabu hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu tabia yake.

''Ukweli ni kwamba nimechukua uamuzi huo ili asiwe nahodha wa pili lakini hakuna tatizo lolote kati yetu'', alisema Mourinho.

''Mimi ndio meneja ninaweza kufanya maamuzi kama hayo''.

Akizungumza na chombo cha habari cha Sky Sports aliongezea: Hakuna tofauti zozote kati yetu ni uamuzi tu ambao sio lazima nieleze.

Kwa nini tuzo za mchezaji bora wa Fifa zatiliwa shaka
Mshindi wa kombe la dunia Pogba 25 aliambiwa kuhusu uamuzi huo kabla ya mechi ya siku ya Jumanne ya kombe la Carabao dhidi ya Derby.

Mourinho amejaribu kuonyesha uzito wake baada ya kosa la Pogba kuisaidia timu ya Wolves kufunga bao la kusawazisha katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumamosi mbali na mchezaji huyo kukosoa mbinu zinazotumika.

Pogba alijaribu kupuuzilia mbali matamshi yake katika mtandao wa twitter siku ya Jumatatu. Lakini katika ripoti yake ya mechi ya Jumanne ambayo Derby ilishinda kwa njia ya penalti , Mourinho alisema kuwa hafurahishwi na baadhi ya wachezaji wake.

''Mechi dhidi ya Wolves ilikuwa funzo zuri , funzo ambalo ninarejelea kila wiki, funzo ambalo baadhi ya wachezaji hawajifunzi'', alisema.

Kila timu inayocheza dhidi ya United hucheza kufa kupona, na tunahitaji kuimarika ili kukabiliana nazo , Asilimia 95 haitoshi iwapo wengine wanatoa asilimia 101.

No comments