Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Rich Mavoko kurudi kivingine zaidi

Msanii wa Muziki Bongo, Rich Mavoko yupo mbioni kuachia wimbo mpya. Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu muimbaji huyo kua...

Rich Mavoko kurudi kivingine zaidi

Msanii wa Muziki Bongo, Rich Mavoko yupo mbioni kuachia wimbo mpya.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu muimbaji huyo kuachia wimbo unaokwenda kwa jina la Asante.

Rich Mavoko ambaye kwa sasa amekuwa si mtumiaji sana wa Instagram, kupitia mtandao huo amewaeleza mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda wowote ngoma mpya inatoka.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya muziki wake chini ya Bilionea Kid ameshaachia nyimbo mbili chini ya lebo hiyo ambazo ni Ndegele na Hongera. Hii ni baada ya kile kinachoelezwa kwa sasa hayupo tena WCB ambapo alijiunga mwaka 2016. 


Follow our Page

No comments