Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

‘TIMUA PAUL POGBA ANAWAZINGUA’

Beki na nahodha wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa mchezo wa soka  amemjia juu kiungo Paul Pogba na k...


Beki na nahodha wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa mchezo wa soka amemjia juu kiungo Paul Pogba na kusema anachangia kuiharibu Manchester United.

Carragher ametoa tamko hilo kufuatia sakata la mgogoro linaloendelea kati ya Pogba na kocha wake, Jose Mourinho ambapo wawili hao hawaelewani huku timu yenyewe ikiwa haifanyi vizuri kwa miezi ya hivi karibuni. 

Pogba alishutumiwa na Mourinho kwa kuweka video akicheka wakati timu hiyo ilipofungwa na Derby Country, Jumanne iliyopita katika Carabao kiasi cha kusababisha wawili hao kurushiana maneno wakiwa mazoezini

No comments