Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

YANGA WAIGOMEA SINGIDA UNITED

Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umeipiga chini ziara ya kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida U...


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umeipiga chini ziara ya kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United.

Yanga ilipanga kuelekea mkoani humo kucheza mechi hiyo ambayo ilipangwa kupigwa Septemba 5 2018.

Taarifa za ndani ya Yanga zinasema, Kocha Mkuu wa timu, Mwinyi Zahera, amegomea safari hiyo na badala yake amehitaji muda na wachezaji kuwaweka fiti zaidi.

Zahera amesema kwa sasa akili na nguvu zote zinapaswa kuelekezwa kwenye ligi ili kufanya vema kwenye mechi zinazokuja mbele yao.

Kocha huyo ameeleza kupania pointi tatu kwa kila mechi ili kuurejesha ubingwa ambao ulichukuliwa na Simba msimu uliopita.

No comments