Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

BAADA YA KUMSAINI ALIKIBA, UONGOZI COASTAL WAFAFANUA KUHUSU KAZI YAKE YA MUZIKI NA MPIRA

Baada ya Coastal Union kufanikiwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja mwanamuziki maarufu nchini, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, uongozi wa timu hiyo ...



Baada ya Coastal Union kufanikiwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja mwanamuziki maarufu nchini, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, uongozi wa timu hiyo umesema hautamzuia kufanya kazi yake ya kuimba.

Kwa mujibu Championi Ijumaa, meneja wa timu hiyo, Said Hilary alisema Ali Kiba ni mchezaji mzuri na ameenda kwenye timu ya mpira na lengo lao kubwa ni kuitangaza Coastal.

“Tumemsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja na tunafahamu yeye ni mwanamuziki kwa hiyo akiwa na shughuli zake za kimuziki ataendelea na shughuli zake kama kawaida na akiwa yupo huru basi atacheza kuisaidia timu maana tuna uamini uwezo wake ndiyo maana tumemsajili,” alisema Hilary.

Usajili huo umekuja kama sapraizi kubwa kwa wadau wa soka kutokana na Kiba kujizolea umaarufu mkubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya huku akisibiriwa kwa hamu na mashabiki wa Coastal Union kuona namna atakavyokuwa anasakata kabumbu.

No comments