Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

GAMBOSHI SEHEMU YA 1

GAMBOSHI SEHEMU YA 1 Baada ya kuwa ametumia miaka miwili nchini Irak akiripoti vita vya Ghuba kupitia televisheni ya SkyNews na kupokea Tu...

GAMBOSHI SEHEMU YA 1

Baada ya kuwa ametumia miaka miwili nchini Irak akiripoti vita vya Ghuba kupitia televisheni ya SkyNews na kupokea Tuzo ya Kimataifa ya Boldness Award iliyoambatana na zawadi ya Dola za Kimarekani milioni moja, mwandishi mahiri wa Kimataifa Richard Massawe, anarejea nchini Tanzania kwa kazi moja tu; kumwoa mwanamitindo na mwanamuziki maarufu wa Kitanzania katika muziki wa Soul, Anitha Johnson.
Wakimaliza kufunga ndoa yao, lengo ni kurejea katika Jiji la Los Angeles, Carlifonia yaliko makazi ya Richard kwenye kitongoji cha Pasadena. Wazazi wake wanafurahi kupita kiasi, kitendo cha kuwaacha wanawake wa Kizungu kwenda kumuoa mwanamke wa Kitanzania kwao ni heshima kubwa, wamejisikia kuheshimiwa. Je, kitatokea nini katika maisha ya watu hawa wawili? Anza hadithi hii ili upate kujifunza maajabu ya nguvu za giza katika kijiji maarufu cha kufikirika cha Gamboshi, kilichopo huko Shinyanga ambako indaiwa kuna watu wanaishi bila kuonekana baada ya kuondoka duniani wakidaiwa kufa.
Ukumbi wa Mwanza hoteli ulikuwa umefurika idadi kubwa ya watu, hapakuwahi kuwa na harusi hata moja iliyowahi kujaza ukumbi huo kama siku hiyo. Ulipambwa kwa maua mazuri ya kuvutia, wapambaji wakiwa ni Kampuni ya Dotnata Decoration ya Dar es Salaam, hakika ukumbi ulivutia, haikuwa rahisi kama mtu angechukuliwa kutoka Uingereza akiwa amefungwa na kitambaa machoni akaingizwa ndani ya ukumbi kisha kitambaa kuondolewa, kuelewa kwamba alikuwa Mwanza, Tanzania.
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania walikuwa wamefurika, kulikuwa na kamera kwenye kila kona, watu wakifuatilia harusi ya mtu maarufu katika tasnia ya habari duniani, aliyetokea Tanzania na kuiitingisha dunia kwa kuripoti mambo mazito yaliyowaogopesha watu wengine.
Baraza zima la Mawaziri lilikuwa limesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kuhudhuria harusi hiyo, kwa harakaharaka mtu angeweza kufikiri kwa kuwepo hapo, labda alikuwa Bungeni Dodoma maana kila mtu alipogeuza shingo kuangalia kushoto na kulia, macho yake yalikutana ama na Waziri kamili au Naibu, hiyo ndiyo ilikuwa picha halisi ndani ya ukumbi wa Makutano.
Watu wote walikuwa wamependeza, wanaume wengi wakiwa ndani ya suti nyeusi na tai za rangi ya pinki, wanawake magauni ya rangi ya maruni yenye kumeremeta, kila kitu ndani ya ukumbi kilikuwa katika rangi zilizopangiliwa sawasawa. Richard akiwa ameketi mbele pamoja na mke wake Anitha ndani ya shela ya kumeremeta iliyonunuliwa kutoka Marekani moja kwa moja tena si dukani bali kwa mbunifu maarufu wa mitindo raia wa Ufaransa aishie Marekani, Pierre Martin aliyeitengeneza maalum kwa ajili ya Anitha!
Macho ya akinamama wengi yalikuwa kwenye vazi hilo lenye kuvutia lililofanana kabisa na Tausi mweupe. Uso wa Anitha ulikuwa umejaa tabasamu, hata yeye hakuamini alichokuwa akikishuhudia mbele ya macho yake, ilikuwa ni sawa na kuota ndoto, maisha yaliyokuwa yakija mbele yake yaliashiria raha mustarehe, hakuwahi kukanyaga Marekani kabla, hivyo pamoja na kuwepo ukumbini akili yake ilikuwa ikifikiria maeneo kama Hollywood, Beverly Hills na kwingineko, alikuwa na uhakika kwa kuingia Marekani peke yake ungekuwa ufunguo wa yeye kufika kwenye umaarufu wa dunia badala ya Tanzania peke yake.
“Thanks God! My dreams are now going to be reality, I am going to be a megastar!” (Namshukuru Mungu! Ndoto zangu zitatimia, sasa nitakuwa nguli wa Kimataifa) aliwaza Anitha akimwangalia mume wake usoni, tabasamu zao zikagongana.
Hapakuwa na mtu asiyemfahamu Anitha nchini Tanzania, alikuwa miongoni mwa watu hamsini maarufu walioitwa The Tanzanian Top 50 Celebrities na kilichomfanya afike alipokuwa maishani mwake ni uanamitindo na kazi yake ya muziki.
Alizaliwa kutoka kwa mama Mtanzania na baba Muingereza, mchanganyiko wake huo wa rangi ulifanya uzuri wake uongezeke! Hakika alikuwa mwanamke mrembo si kwa sura tu bali pia umbile lake ambalo wengi waliliita namba sita, nyuma akiwa ameumbika kisawasawa.
“Hakika ameoa mwanamke mzuri, sikuwahi kufikiria hata siku moja kuna wanawake warembo kiasi hiki huku Afrika!” mmoja wa wageni kutoka Marekani alimwambia mwenzake.
“Sio utani, binti kaumbika, utafikiri namwangalia Alicia Keys au Beyonce? Siamini!”
“Ndio maana Richard alikimbilia huku kuoa, Marekani yote hakuona!”
“Kweli kabisa”
Maongezi ya watu hao yalikatishwa na sauti ya MC aliyekuwa akimkaribisha Anitha ukumbini, katika ratiba kulikuwa na sehemu ambayo alitakiwa kumwimbia mume wake wimbo maalum. Watu wote wakatulia kusubiri, Richard akamnyanyua mke wake taratibu kutoka kitini na kumuongoza hadi katikati ya ukumbi ambako alikabidhiwa kipaza sauti na kukohoa kidogo kisha kuendelea;
“This song is a dedication to my dear husband Richard, I love you so much and nothing gonna change my love for you!” (Wimbo huu ni maalum kwa mume wangu mpendwa Richard, nakupenda sana na penzi langu kwako halitabadilika!) akaongea na ukumbi ukafunikwa ka vifijo, nderemo na vigelegele, ilikuwa ni shangwe ya ajabu, midundo ya wimbo uitwao Nothings Gonna Change My Love For You wa George Benson ilianza kusikika na Anitha akaanza kuimba:
If I had to live my life without you near me
The days would all be empty
The nights would seem so long
With you I see forever oh, so clearly
I might have been in love before
But it never felt this strong
Our dreams are young and we both know
They’ll take us where we want to go
Hold me now, touch me now
I don’t want to live without you.
Chorus 1
Nothing's gonna change my love for you
You oughta know by now how much I love you
One thing you can be sure of
I’ll never ask for more than your love.
If the road ahead is not so easy
Our love will lead the way for us, like a guiding star
I’ll be there for you if you should need me
You don’t have to change a thing
I love you Richard just the way you are.
(Kama ningetakiwa kuishi maisha bila wewe karibu yangu,
Siku zote zisingekuwa na cha maana,
Usiku ungeonekana mrefu kuliko kawaida,
Nikiwa na wewe naona milele waziwazi,
Inawezakana nilishapenda kabla,
Lakini halikuwa penzi zito kiasi hiki
Ndoto zetu bado ni changa, sote tunafahamu,
Lakini zitatupeleka tunakotaka kwenda,
Nikumbatie, niguse sasa,
Sitaki kuishi bila wewe,
Kiitiko;
Hakuna kitakachoweza kubadilisha penzi langu kwako,
Unatakiwa kufahamu tangu sasa ni kiasi gani nakupenda,
Kitu kimoja lazima unaweza kuwa na uhakika nacho,
Sitakuomba kitu chochote zaidi ya penzi lako,
Kama njia mbele yetu itakuwa ngumu,
Penzi letu litatuonyesha njia kama nyota kiongozi,
Nitakuwepo kwa ajili yao, kama utanihitaji,
Hauhitaji kubadili kitu chochote,
Nakupenda Richard ulivyo, si kwa chochote bali jinsi ulivyo…)
Anitha aliimba kwa sauti ya kasuku, akionyesha hisia kali, ukumbi ulikuwa kimya, hakuna aliyeshangilia maneno aliyokuwa akiimba yaliwachoma watu mioyoni, alikuwa akiusema moyo wake! Richard alishindwa kuvumilia akamnyanyua asiendelee kupiga magoti mbele yake, machozi yalikuwa yakimbubujika, hata yeye alimpenda Anitha kuliko kitu kingine chochote, wakakumbatiana! Hapohapo miale ya mwanga wa kamera za wapigapicha ilimulika, kwa muda wa karibu dakika kumi waliendelea kukumbatiana huku vigelegele vikisikika ukumbini, walipoachiana walitazamana na kutabasamu.
“I love you Anitha!” (nakupenda Anitha)
“Nakupenda pia Richard!”
Je, nini kitaendelea?

No comments