Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Ni wiki nyingine ya rekodi kubwa kwa Drake

Drake aliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 Mei 23, 2009 na wimbo wake 'Best I Ever Had.' Mpaka sasa nd...

Drake aliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 Mei 23, 2009 na wimbo wake 'Best I Ever Had.' Mpaka sasa ndio msanii (Solo Artist) ambaye anaongoza kwa kuingiza nyimbo nyingi kwenye chati hizo, ameingiza nyimbo 186, Drizzy pia anaishikilia rekodi ya kuingiza nyimbo nyingi kwa wiki, ameingiza nyimbo 27.

Ni wiki nyingine ya rekodi kubwa kwa Drake, Rapper huyo amebakiza jumla ya namba 16 tu ili awe amekalia/ameshika kila namba (nafasi) kwenye chati za Billboard Hot 100 tangu aingie rasmi kwenye chati hizo Mei 23, 2009.

Namba zilizobaki ni pamoja na: 11, 19, 22, 31, 34, 39, 43, 46, 59, 66, 77, 85, 93, 96, 98 na 99, ndio namba (nafasi) pekee ambazo drake hajawahi kushika lakini zingine zote (84) zilizobaki amezikalia kwa nyimbo tofauti tofauti ikiwemo za kushirikishwa.

Nyuma yake wapo Glee Cast ambao wana rekodi ya kushika namba/nafasi 80 kati ya 100 na Lil Wayne anafatia akiwa amezikalia nafasi 72 kati ya 100.

Drake aliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 Mei 23, 2009 na wimbo wake 'Best I Ever Had.' Mpaka sasa ndio msanii (Solo Artist) ambaye anaongoza kwa kuingiza nyimbo nyingi kwenye chati hizo, ameingiza nyimbo 186, Drizzy pia anaishikilia rekodi ya kuingiza nyimbo nyingi kwa wiki, ameingiza nyimbo 27.

RNGM blog

No comments