Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Peter wa P Square aibua mapya kuvunjika kwa kundi lao

Paulo mara zote hakuheshimu familia yangu, kwa hiyo nilitolea kuwalinda, amesema Peter aliyekuwa akiunda kundi la P Square. Pet...











Paulo mara zote hakuheshimu familia yangu, kwa hiyo nilitolea kuwalinda, amesema Peter aliyekuwa akiunda kundi la P Square.

Peter Okoye kwa sasa hayupo katika kundi la muziki la P Square, hatimaye ameelezea kwa nini alisimama kufanya muziki pamoja na ndugu yake wa mapacha, Paul.

Akizungumza na Citizeni TV nchini Kenya, Peter alisema;  "Katika maisha familia ni kitu cha muhimu chenye dhamani. Mashabiki wanataka P Square lakini mara ngapi unataka P Square kurudi na kuvunja?". 

"Tumevunja mara tatu na suala hilo liko bado. Kwa hiyo ikiwa Psquare itarudi tunahitaji kushughulikia suala hilo, P Square inaweza kurudi au isirudi," amesisitiza Peter. 

Ameendelea kwa kusema alijitoa kwa sababu alihisi kutokuheshimu kungekuja hata kwenye familia yake kitu ambacho kilikuwa kimeshazidi.

"P Square inaweza kurudi tu ikiwa heshima inakuwepo kwa asilimia 100. Mimi siheshimu mke wa kaka yangu na familia yake lakini anafanya hivyo kwangu wakati wote. Yeye atanilaumu mimi na familia yangu kwa umma, kwenye Instagram, na dakika ya pili atanisubiri backstage ili kutumbuiza!," amesema.

"Siwezi kufanya hivyo, jambo moja ni kwa hakika, nilitimiza dhamana ya kumlinda mke wangu na watoto na siku niliyofunga ndoa niliahidi kusimamia hilo," amesisitiza Peter Okoye.


RNGM blog

No comments