Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

UTAPELI MPYA WA KU-SWAP LAINI ZA SIMU UNAVYOFANYIKA

Kwa Watanzania wote wanaoutumia simu za mkononi, hii ni kwa ajili yenu na naomba uwe makini uisome habari hii na kuielewa. Huu ni wizi...




Kwa Watanzania wote wanaoutumia simu za mkononi, hii ni kwa ajili yenu na naomba uwe makini uisome habari hii na kuielewa.
Huu ni wizi mpya wa kutumia teknolojia ambao umeingia mjini kwa kitaalamu wanauita “Swim Swap Fraud” na kuna baadhi ya watu katika eneo letu la Afrika Mashariki tayari wameshalizwa.
Jinsi unavyofanya kazi
1
Mtandao kwenye simu yako unapotea ghafla, unaona imeandika “No Signal au Zero Bars” halafu baada ya muda unaona simu inaingia.
2
Hiyo namba iliyokupigia simu unakuwa huifahamu na inaweza kuwa ya mtandao wowote Tigo/Airtel/Halotel/TTCL/Vodacom na kadhalika kutegemea unatumia mtandao upi ambao muda huo sasa ndio unakuwa umekumbwa na hiyo shida ya kupotea potea kwa mtandao.
3
Huyo aliyepiga anatakuambia kwamba kuna tatizo la mtandao kwenye simu yako na wewe utakubali kwa sababu kweli kuna tatizo. Atakuelekeza kubonyeza 1 ili tatizo la mtandao kwenye simu yako liweze kutatuliwa.
Akikupa maelekezo hayo usifanye lolote, kata simu. 
Kwa sababu  utakapobonyeza 1, mtandao wako utarudi ghafla na kisha kupotea (zero bars) na kwa kitendo hicho simu yako inakuwa imedukuliwa (hacked).
Wizi huu unaongezeaka siku baada ya siku na kama una fedha kwenye akaunti yako ya simu (Tigo Pesa, Airtel Money, etc) basi zote zinatolewa.
Baada ya tukio hilo wewe utaona tu simu yako shida ni kwamba haina network lakini tayari wakati huo line yako ya simu inakuwa swapped na taarifa zote kwenye line yako anakuwa nazo huyo aliyefanya tukio. Tatizo hapa ni kwamba hutapata taarifa zozote za kufanya kwa miamala ya aina yoyote kupitia simu yako kwa hiyo kwa wale wanaotumia USSD na Mobile Banking kuweni makini.

No comments