Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

LIONEL MESSI KUMFUATA RONALDO

Vita kali ya mafanikio kati ya mahasimu wa soka  duniani, Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa barcelona haijafika kikomo baad...



Vita kali ya mafanikio kati ya mahasimu wa soka  duniani, Cristiano Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa barcelona haijafika kikomo baada ya wawili hao kutajwa kurudi kwenye ligi moja ya Italia ‘Seria A’

Ronaldo ambaye hivi karibuni alihama Real Madrid ya Hispania na kujiunga Juventus ya Italia, imeonekana kama ametengana na mpizani wake Messi aliyebaki nchini Hispania katika Klabu ya Barcelona, lakini huwenda mambo yakawa sivyo kwa wawili hao kukutana tena kwenye ligi moja ambayo ni Serie A ya nchini Italia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Italia klabu ya Inter Milan inahusishwa kutaka kumsajili mshambuliaji hatari wa Barcelona, Lionel Messi ili kuleta ushindani kwenye ligi ya Serie A dhidi ya Juventus ambao wamekamilisha dili la kuingia kandarasi na Cristiano Ronaldo.

Wadhamini wakuu wa Inter Milan ambao ni kampuni ya Pirelli kupitia Mkurugenzi mtendaji wake, Marco Tronchetti Provera wamesema mmiliki wa timu hiyo ambayo ni Suning chini ya Zhang Jindong inatarajia kufanya usajili mkubwa mno kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Tronchetti amesema haaimani kama Suning inaweza kufanya usajili mkubwa sana na kuhoji kwa nini isiwezekane kuwa ni Messi ambaye ameingia mkataba wa muda mrefu na klabu ya Barcelona unaomuweka hapo mpaka msimu wa mwaka 2021.

No comments