Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MFAHAMU MTUNZI WA “TUNE” YA WIMBO WA TAIFA “MUNGU IBARIKI TANZANIA”

Kwa wale ambao wamesafiri nchi za kusini mwa Afrika kama Zambia na Afrika Kusini watakuwa wamegundua kwamba mbali na tofauti ya mashairi...




Kwa wale ambao wamesafiri nchi za kusini mwa Afrika kama Zambia na Afrika Kusini watakuwa wamegundua kwamba mbali na tofauti ya mashairi, nyimbo za mataifa ya Afrika Kusini, Zambia na Tanzania zinafanana “tune”, au mapigo na mtiririko wa ala.
Utunzi huo ambao hadi leo unatumika katika nyimbo za mataifa hayo ulifanywa Enoch Mankayi Sontonga, raia wa Afrika ya Kusini na mzaliwa Uitenhage katika Jimbo la Cape Mashariki. Sontonga alizaliwa mwaka 1873. Alitokea kabila la Xhosa na alipata mafunzo ya Ualimu na kuhitimu katika Chuo cha Lovedale. Baada ya kuhitimu alipata ajira kama mwalimu na mkufunzi wa kwaya kwenye shule ya wamisionari wa Methodist kwenye eneo la Nancefield nje kidogo ya Jiji la Johannesburg. Alidumu shuleni hapo kwa miaka minane. 
Ubeti wa kwanza wa tuni hii (Nkosi Sikelel’ iAfrika/Mungu Ibariki Afrika) uliandikwa mwaka 1897 na mwanzo alikusudia uwe tu wimbo wa shule. Baadhi ya vyanzo vinasema hata tuni nzima ya wimbo iliandikwa mwaka huo huo wa 1897. Tuni nzima iliimbwa kwa mara ya kwanza mwaka 1899. Chama tawala Afrika Kusini (ANC) kilianza kuutumia katika harakati zake za kudai uhuru mwaka 1925.
Enoch Mankayi Sontonga
Alifariki dunia Aprili 18, 1905 Jijini Johannesburg, akiwa na umri wa miaka 32. Septemba 24 mwaka 1996 (miaka 91 baada ya kilo chake) kaburi lake lilitangazwa kuwa moja ya minara ya kumbukumbu za kitaifa nchini Afrika Kusini.

No comments