Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

JPM amrudisha Jokate Instagram baada ya miezi 3; Post yake ya kwanza hii hapa!

Siku ya jana July 28, 2018 Rais Dk. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali, miongoni mwa walioteuliwa ...










Siku ya jana July 28, 2018 Rais Dk. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali, miongoni mwa walioteuliwa ni Mwanamitindo na Mjasiriamali, Jokate Mwegelo.

Kwa mara ya kwanza mrembo huyo amezungumzia uteuzi wake kwa kirefu zaidi. Kupitia Instagram hiki ndio kile alichoandika; 

Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu.

Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi. 

Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. 

Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako. Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu. .
.
Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni 🙏🏽


Ujumbe wa Jokate unakuja siku moja baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kisarawe. Tangu April 19, 2018 mrembo huyo alikuwa hajaposti chochote katika ukurasa wake wa Instagram wenye followers zaidi ya Milioni 3.1.

RNGM blog

No comments