Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Bill Nass amshauri Steve Nyerere kufungua kampuni ya kusimamia misiba

Msanii wa Bongo Flava, Bill Nass amemshauri muigizaji Steve Nyerere kufungua kampuni ya kusimamia misiba kwa sababu ni kazi an...















Msanii wa Bongo Flava, Bill Nass amemshauri muigizaji Steve Nyerere kufungua kampuni ya kusimamia misiba kwa sababu ni kazi anayoiweza zaidi.

Bill Nass akipiga stori na Wasafi TV amesema kuliko Steve Nyerere kutumia fedha zake kuandaa event za comedy ni bora akafanya hivyo na anaweza kupata fedha nyingi zaidi.

"Kuliko kuwekeza fedha zake sijui kuandaa comedy kubwa anaweza akafungua kampuni za kushughulika na misiba na akatengeneza fedha," amesema Bill Nass. 

"Anaweza akatumia mtaji huo huo mdongo akanunua gari za kubebea maiti, akawa na vitu ambavyo vina-deal na hiyo fild kwa sababu anaiweza sana," ameongeza.

Bill Nass kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Labda. 


RNGM blog

No comments