MKUU wa Wilaya ya Arumeru ambaye aliwahi kuwa ofisa habari wa Yanga Jerry Muro ameshangaa wanaodai timu yao ni dhaifu. “Nani anasema Yanga...
MKUU wa Wilaya ya Arumeru ambaye aliwahi kuwa ofisa habari wa Yanga Jerry Muro ameshangaa wanaodai timu yao ni dhaifu.
“Nani anasema Yanga mbovu, Yanga ni bora msimu huu kuliko timu yoyote wala isipimwe uwezo wake kwenye hizi mechi mbili tatu kwani itakuja kufanya balaa siku za usoni,” alisema Muro.
Straika mwenye nafasi kwenye kikosi cha kwanza, Juma Balinya nae akaongeza kwamba; “Mpira siku zote una matokeo tofauti, wakati mwingine unaweza ukapata matokeo chanya na muda mwingine unapata matokeo hasi kwahiyo mashabiki wanapaswa kuyakubali matokeo haya.”
“Wanachotakiwa kuamini ni kwamba mambo mazuri yanakuja hivyo wasiwe na wasiwasi,” alisema Balinya ambaye ni raia wa Uganda.
No comments