Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

REKODI ZA WALIOTWAA NGAO YA JAMII BONGO ZPO NAMNA HII

MCHEZO wa ngao ya Jamii ambao huwakutanisha mabingwa wawili tofauti   umeacha rekodi ya aina yake kwa timu zote mbili ambazo zilicheza ...


MCHEZO wa ngao ya Jamii ambao huwakutanisha mabingwa wawili tofauti umeacha rekodi ya aina yake kwa timu zote mbili ambazo zilicheza mchezo huo.

Agosti 17, Simba ilimenyana na Azam FC kwenye bonge moja ya mchezo wa ngao ya jamii ulioshuhudia wanaume 22 wakipambania Ngao ya Jamii.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara walimenyana na Azam FC ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Uwanja wa Taifa ulishuhudia jumla ya mabao sita yakifungwa idadi kubwa ya mabao ndani ya dakika 90 kwenye jumla ya michezo 12 ambayo imechezwa mpaka sasa.

Azam FC walikubali kufungwa jumla ya mabao 4-2 licha ya wao kutangulia kufungua njia kupitia kwa Idd Chilunda dakika 13 ambaye alifunga bao hilo akimalizia pasi ya John Richard kwa guu la kushoto.

Dakika ya 16 Hassan Dilunga kiungo wa Simba aliachia mkwaju wa moto akiwa nje ya 18 uliotemwa na Razack Abarola mlinda mlango wa Azam FC ukakutana na kichwa cha Sharaf Eldin Shibob aliyeuzamisha nyavuni mpira.

Shiboub tena aliwanyanyua mashabiki wa Simba akimalizia pasi ya Mohmed Hussen, ‘Tshabalala’

Clatous Chama aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa kuwachambua mabeki wa Azam FC na kupachika bao la tatu dakika ya 57 kwa guu lake la kushoto.

Frank Domayo dakika ya 78 alifunga bao la kideo kwa upande wa Azam FC akimalizia pasi ya Obrey Chirwa
Msumari wa nne ulikomelewa na Francis Kahata dakika ya 88 akiwa ndani ya 18 kwa guu lake la kushoto na kushangilia kwa mtindo wa kuchechemea.

Ngao ya jamii ambayo ilianzishwa mwaka 2001 kabla ya kusitishwa na kurudishwa tena mwaka 2009 imeshuhudia Simba na Yanga zikiwa zimetoshana nguvu kutwaa zikitwaa zote mara tanotano huku Mtibwa na Azam FC zikitwaa mara mojamoja, mabingwa wapo namna hii:-


2001: Mshindi wa Kwanza alikuwa Yanga alishinda mbele ya Simba kwa ushindi wa mabao 2-1

Mabao ya Yanga yalifungwa na Edbly Lunyamila na Ally Yussuph na bao la Simba likipachikwa na Steven Mapunda.

2009 Mtibwa Sugar
Ilishinda bao 1-0 dhidi ya Yanga

2010
Yanga 3-1 Simba
Yanga lishinda kwa penalti baada ya dakika 90 kutoka Sare ya kutofungana

Mabao ya Yanga yalipachikwa na marehemu Geoffrey Bonny, Stephano Mwasika na Isack Boakye, kwa Simba Mohamed Banka ndiye aliyefunga Emmanuel Okwi Uhuru Seleman, Juma Nyosso walikosa penalti

2011
Simba 2-0 Yanga

Wafungaji kwa upande wa Simba walikuwa ni Haruna Moshi na Felix Sunzu.

2012
Simba 3-2

Mabao kwa Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi, Daniel Akuffor na Mwinyi Kazimoto yale ya Azam yalipachikwa na John Bocco na Kipre Tchetche.

2013

Yanga 1-0 Azam
Bao likipachikwa na Salum Telela

2014 Yanga 3-0 Azam
Gerson Santos 'Jaja'

2015 Yanga 8-7 Azam Penalty

Dakika 90 Sare ya bila kufungana

Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amiss Tambwe, Andrey Coutinho, Geoffrey Mwashiuya, Thaban Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondani.
Kwa Azam Kipre Tchetche, John Bocco, Himid Mao, Aggrey Morris, Jean Baptist, Mugiraneza, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe

2016 
Azam FC 4-1 Yanga penalti

Dakika 90 walifungana mabao 2-2
Mabao ya Yanga yalifungwa na Donald Ngoma huku Kwa Azam Kapombe na Bocco.

Penalti Kwa Azam FC zilifungwa na Kapombe, Michael Ballou, Himid Mao na John Bocco Yanga mfungaji alikuwa Deogratius Munish 'Dida'.

2017

Simba 5-4 Yanga
Dakika 90 ilikuwa Sare ya bila kufungana.
Method Mwanjali, Haruna Niyonzima, Okwi, Shiza Kichuya na Mohamed Ibrahim na Yale ya Yanga yalifungwa na Papy Tshishimbi, Thaban Kamusoko, Ibrahim Ajibu na Donald Ngoma

 2018 Simba 2-1 Mtibwa
Mabao ya Simba Meddie Kagere na Hassan Dilunga na lile la Mtibwa lilifungwa na Kelvin Sabato.

2019
Simba 4-2 Azam FC

Shiboub mabao 2, Chama na Kahata mojamoja kwa upande wa Simba na Chilunda na Frank Domayo Kwa Azam FC.

No comments