Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

KMC YAPANIA KUFANYA KWELI KESHO TAIFA KIMATAIFA

JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kikosi kipo imara kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya AS Kigali utakaochezwa uwanja...


JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kikosi kipo imara kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya AS Kigali utakaochezwa uwanja wa Taifa.

KMC kesho ina kibarua mbele ya AS Kigali ya Rwanda kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho baada ya ule wa awali kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana.

 Mayanja amesema mchezo utakuwa wa wazi na wamejipanga kupata matokeo chanya licha ya kutokuwa na washambuliaji halisi.

"Kuna baadhi ya majeruhi ambao wapo kwetu jambo linalotuumiza ila hakuna tatizo ni mchezo wetu.

"Hatuna mshambuliaji kamili kwa sasa kutokana na majeruhi yanayowasumbua, mchezaji kama Aiyee (Salim) kwa sasa hayupo sawa ila tumejipanga kufanya vizuri kikubwa sapoti," amesema.

No comments