Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MANULA FITI KUWAVAA UD SONGO KIMATAIFA

MLINDA mlango namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula ameanza mazoezi ndani ya kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ...


MLINDA mlango namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula ameanza mazoezi ndani ya kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya UD Songo, Jumapili uwanja wa Taifa.

Manula alikuwa anatibu majeraha yake ya nyonga na amekosa mechi mbili za mashindano ambazo zote langoni alikaa Beno Kakolanya.

Manula amesema kuwa hana mashaka na uwezo wa Kakolanya hivyo mwalimu ndio anajua nani aanze kwakwe yeye hana tatizo.

"Wachezaji wote ndani ya Simba ni bora na wanajua kazi yetu ni kutafuta matokeo chanya, hivyo akianza Kakolanya ama Salim wote kazi yetu ni moja," amesema.

Huenda akawavaaa UD Songo, kwenye mchezo marudio utakaopigwa uwanja wa Taifa Jumapili.

No comments