Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

NIYONZIMA AREJEA SIMBA

KIUNGO wa zamani wa Simba na Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa hakuna timu yoyote yenye uwezo wa kuifunga Simba ikiwa inacheza kwenye U...


KIUNGO wa zamani wa Simba na Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa hakuna timu yoyote yenye uwezo wa kuifunga Simba ikiwa inacheza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Niyonzima ameyasema hayo ikiwa Simba ipo kambini ikijiandaa kuvaana na UD do Songo katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Niyonzima amesema ameiona Simba mpya na kukiri kuwa ipo vizuri na ana imani itafanya vizuri msimu huu, huku akiongeza kwamba hakuna timu itakayoweza kuizuia kupata
ushindi ikiwa ndani ya uwanja wao wa nyumbani.

“Simba ni timu nzuri tangu msimu uliopita lakini kwa awamu hii nimeona mabadiliko ya wachezaji ambao wengi ni wazuri pia na wanaweza wakaisaidia Simba kufanya vizuri zaidi, sidhani kama kuna timu itaweza kuifunga Simba ikiwa Uwanja wa Taifa,” alisema Niyonzima.

Kauli ya Niyonzime imekuja baada ya kutembelea mazoezi ya wekundu hao wa Msimbazi alipoenda kuwasalimia baada ya kuitumikia msimu uliopita.

Niyonzima alikuwepo nchini na timu ya AS Kigali kwa ajili ya mechi na KMC japo hakucheza kutokana na kukosa kibali cha CAF.

No comments