Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Van Persie atoa sababu kuitosa Arsenal kutua Manchester United

Mkongwe Robin van Persie amefichua sababu kubwa iliyomfanya aipige chini Arsenal na kwenda kujiunga na Manchester United. Fowadi huyo wa ...


Image result for vanpersie discuss about arsenal

Mkongwe Robin van Persie amefichua sababu kubwa iliyomfanya aipige chini Arsenal na kwenda kujiunga na Manchester United.
Fowadi huyo wa Kidachi alionekana msaliti na mashabiki wa Arsenal kutokana na uamuzi wake huo wa kuhamia Man United kwa ada ya Pauni 24 milioni, Agosti 2012.
Kipindi kile, Van Persie, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 36 na ameshastafu soka, aliandika barua ndefu kwa mashabiki wa Arsenal kuhusu kuondoka kwake, lakini hakuweka wazi sababu iliyomfanya achukue uamuzi huo. Lakini, sasa kwa mara ya kwanza, akiwa mchambuzi wa BT Sport ameamua kuweka wazi sababu nzima.
"Unaweza kulinganisha maisha yang na Arsenal ni kama ndoa. Mimi na mke wangu - Arsenal - tulioana kwa kipindi cha miaka minane. Baada ya miaka minane, mke wangu, ameamua kunichoka. Hivyo ndivyo ilivyokuwa," alisema RVP.
"Kama Arsenal hawakupi mkataba mpya...unaweza kuwa na mtazamo tofauti, lakini ukweli ni kwamba Arsenal hawakunipa ofa ya mkataba mpya. Hivyo nikaamua kutazama kwingineko. Na hapo bado nilikuwa nataka kushinda ubingwa wa ligi kwenye maisha yangu.
"Nikawa na sehemu tatu za kuchagua. Sehemu moja ya nje ya England ikayeyuka, nikawa nimebaki na ama kwenda Manchester City au Manchester United. Kitu ambacho watu hawakifahamu kuhusu uhamisho, mambo mengi yanayokea nyuma ya pazia huko. Nilizungumza na Wenger na Ivan Gazidis. Hawakuwa na uamuzi."
Van Persie amemaliza kwa kusema kwamba hata baada ya kuhama wala hakuwa na hisia yoyote mbaya kuhusiana na Arsenal.

No comments