Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MENEJA WA MACHESTER UNITED AMKINGIA KIFUA POGBA

MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajaer amesema kuwa hakuna tatizo kwa kiungo wake Paul Pogba kushindwa kufunga penalti kwani n...


MENEJA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajaer amesema kuwa hakuna tatizo kwa kiungo wake Paul Pogba kushindwa kufunga penalti kwani ni sehemu ya mchezo.

Manchester United ilikubali kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Wolves licha ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wao wa pili wa Premier League.

Manchester United walianza kufunga bao kupitia kwa Anthony Martial dakika ya 27 kabla ya Wolves kuweka usawa dakika ya 55 kupitia kwa Ruben Neves dakika ya 55.

"Kwangu mimi sioni tatizo kwake kushindwa kufunga ni sehemu ya mchezo na inatoa nafasi ya kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu mwingine.

"Nina wapigaji wawili wa penalti ambao ni Pogba na Rashford kwa kuwa yeye amepiga hakuna shida," amesema.

Mchezo wa kwanza United ilipata ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Chelsea uwanja wa Old Trafford. 

No comments