Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

KERR AWAJIA UPYA SIMBA

Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Muingereza, Dylan Kerr, amesema usajili wa kiungo Francis Kahata ambaye ni raia wa Kenya, utai...



Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Muingereza, Dylan Kerr, amesema usajili wa kiungo Francis Kahata ambaye ni raia wa Kenya, utaisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Kerr amefunguka kwa kusema anamjua vema Kahata kuliko hata Simba wenyewe sababu amemfundisha kwa muda mrefu wakati akiinoa Gor Mahia FC ambayo Kahata alikuwa akiichezea.

Kerr ambaye yupo kwao England akiwa hana timu, anaamini uwepo wa Kahata utazidi kuifanya Simba iwe bora haswa anapocheza na Meddie Kagere ambaye naye alimfundisha wakati akiwa Gor Mahia.

"Usajili wa Kahata ni mzuri na utaboresha kikosi cha Simba kwani ni mzuri katika kumiliki mipira na hapotezi kirahisi, nimekuwa naye kwa muda mrefu na namfahamu.

"Uwepo wake utaifanya Simba izidi kuwa bora haswa kwenye idara ya kiungo, na akicheza na Kagere ambaye nilimfundisha nikiwa Gor Mahia, naamini kabisa timu itakuwa na makali.

"Sifa moja ya Kahata ni mtulivu na anaweza kutulia na mipira, anagawa pasi na zinafika kwa wenzake, kwakweli Simba wamelamba dume pale," amesema Kerr.

Kwa upande mwingine Kerr ambaye anafuatilia mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, amewashauri Simba kuhakikisha wanaongeza makali kwenye nafasi yao ya ulinzi ili kuzuia mabao kabla ya mechi na UD Songo ambayo wanacheza nayo leo jioni saa 10 kamili.

Ameeleza ili kuifanya timu iwe na rekodi nzuri ni vema ikahakikisha nyavu zake haziguswi, tofauti na msimu uliopita ilivyoruhusu mabao mengi haswa katika mechi za kimataifa za Ligi ya Mabingwa.

"Simba wanapaswa kutoruhusu mabao mengi langoni mwao, niliona msimu uliopita walikuwa na tatizo kubwa kwenye ulinzi, hilo vema wakalizingatia," alisema.

No comments