Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa Ngao ya Hisani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa kwenye...
Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa Ngao ya Hisani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza leo.
Simba imeibuka na ushindi huo kupitia mabao ya Meddie Kagere aliyefunga mnamo dakika ya 29 na Hassan Dilunga kwenye dakika ya 45 kuelekea mapumziko.
Bao pekee la Mtibwa limepachikwa kimiani na Kelvin Sabato kwa mpira wa shuti kali aliopiga nje kidogo ya eneo la 18 upande wa kulia na kumuacha Kipa Aishi Manula akiwa hana la kufanya.
Ubingwa huo wa Simba ni ishara nzuri ya kuanza msimu ujao wakiwa na taji moja huku Kocha wake mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems akifanikiwa kulitwaa kwenye mechi yake ya kwanza kiushindani.
Kikosi hicho kitaanza harakati za kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara Agosti 22 kitapoanza kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
No comments