Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

NDITI AZIDI KUWAPA PRESHA SIMBA

Wakati Simba na Mtibwa Sugar zikishuka dimbani Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza leo kwa ajili ya mchezo wa kuwania Ngao ya Hisani, Nahodha ...


Wakati Simba na Mtibwa Sugar zikishuka dimbani Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza leo kwa ajili ya mchezo wa kuwania Ngao ya Hisani, Nahodha wa Mtibwa, Shaban Nditi, amefunguka mambo kadhaa kabla ya kuwavaa wapinzani wao.

Nditi amesema kuwa katika mpira hakuna mchezaji wa ugenini wala ndani bali wanaume 22 watakaoingia Uwanjani ndiyo watakaoamua matokeo ya mechi.

Mkongwe huyo aliyewahi kuwa Nahodha wa timu ya taifa 'Taofa Stars' kwa miaka kadhaa nyuma, anaamini mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na timu zote mbili kufanya maandalizi ya kutosha.

Nditi mwenye heshima kubwa ndani ya kikosi cha Mtibwa amelizungumzia hilo kutokana na Simba kuwa na wachezaji wengi wanaotoka nje ya Tanzania wakati Mtibwa ikiwa na wazawa.

"Kwenye mpira hakuna mchezaji wa nje wala ndani, wanaume 22 watakaingia Uwanjani wataamua matokeo japo mchezo utakuwa mgumu" alisema.

No comments