Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Kocha Mtibwa apania kuiduwaza Simba

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wanahitaji kuweka rekodi katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simb...
















Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wanahitaji kuweka rekodi katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba hapo kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari mchana huu, Katwila amesema mchezo huo ni muhimu kwao kuweka rekodi ya kuwafunga Simba na kubeba ubingwa wa kombe hilo.
"Wachezaji wote (20) wapo fiti hata waliobaki Morogoro nao hawana tatizo kikubwa nataka tushinde huo mchezo na tumejiandaa kuweka rekodi" alisema Katwila.
Nahodha wa Simba, John Bocco alisema wataingia mchezoni bila historia kutokana na Uwanja wa Kirumba kupata matokeo kwa mbinde.
"Hatuingii uwanjani kwa historia, tunachotaka ni ushindi ili kuanza rasmi msimu wa Ligi Kuu" alisema Bocco.
Nahodha huyo ameongeza kuwa anawashukuru wadau na mashabiki ambao wamejitokeza kwa wingi kuwapokea na kuahidi furaha waliyowaonyesha kwenye mapokezi wajitokeze uwanjani.

No comments