Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

NYOTA SERENGETI BOYS AHITAJIKA MANCHESTER UNITED

Baada ya kuonesha kipaji maridhawa kwa mechi kadhaa alizochezwa, imeelezwa kuwa uongozi wa Manchester United kupitia wakala wake umeanza h...


Baada ya kuonesha kipaji maridhawa kwa mechi kadhaa alizochezwa, imeelezwa kuwa uongozi wa Manchester United kupitia wakala wake umeanza harakati za kuwania saini ya mshambuliaji, Kelvin John anayekipiga Timu ya Taifa ya Vijana (U17), Serengeti Boys.

John ambaye yupo katika mashindano ya CECAFA na timu hiyo, aliibuka kidedea katika mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda kwa kufunga mabao matatu pekee katika ushindi wa mabao 4-0.

Taarifa imeeleza kuwa kigogo mmoja kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hakutaka jina lake kuwekwa wazi, alisema tayari mazungumzo yameshaanza baina yake na wakala huyo kwa ajili ya kumsajili John.

Kiongozi huyo amesema kinachofanyika sasa hivi ni mazungumzo ili kujua faida ya pande hizi mbili kama watakuja kufikiana mwafaka basi anaweza akaelekea United.

Aidha, mbali na United, imeelezwa pia baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zimevutiwa naye na zimeshaanza mazungumzo ya kimyakimya kuhakikisha zinapata saini yake

No comments