Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

KINACHOSUBIRIWA YANGA MPAKA SASA NI HIKI

Wakati wadau na mashabiki wa soka wakisubiria kwa hamu kuitazama Yanga kesho ikimenyana na USM Alger, uongozi wa klabu hiyo umesema maanda...



Wakati wadau na mashabiki wa soka wakisubiria kwa hamu kuitazama Yanga kesho ikimenyana na USM Alger, uongozi wa klabu hiyo umesema maandalizi ya kuwavaa waarabu yapo tayari.

Yanga wamesema baada ya kuweka kambi ya wiki mbili mjini Morogoro na kucheza mechi kadhaa za kirafiki wanaamini muda ukifika wataonesha upinzani mkubwa na USM kwenye mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza mpaka sasa hakuna mchezaji yoyote ambaye ni majeruhi hivyo hilo nalo litachangia kwa namna moja ama nyingine kwa Yanga kupata matokeo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema wachezaji wote wapo fiti na hakuna ambaye ana matatizo ya kiafya kwa ajili ya kipute hicho ambacho Yanga itakuwa itakuwa inawakilisha taifa.

Ikumbukwe katika mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga iliambulia kipigo cha aibu huko Algiers Algeria kwa kufungwa mabao 4-0 na mpaka sasa ina alama moja pekee kwenye kundi D.

No comments