Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Kisa Modric

Real Madrid imeishtaki Inter Milan kwa Fifa kwa madai ya kujaribu kumshawishi kiungo wao Luka Modric ajiunge nao. Kiungo huyo mwenye...

Image result for modric inter
Real Madrid imeishtaki Inter Milan kwa Fifa kwa madai ya kujaribu kumshawishi kiungo wao Luka Modric ajiunge nao.
Kiungo huyo mwenye miaka 32, alikuwa nahodha wa Croatia katika Kombe la Dunia ambako alitajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo, amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Serie A msimu huu.
Rais wa Real, Florentino Perez alisema mapema mwezi huu kuwa njia pekee ya kuondoka kwa Modric ni pale atakapolipiwa dau la euro 750 milioni ambayo ndiyo thamani ya mkataba wake.
Miamba hiyo ya Hispania imemuuza nyota wake mwingine Cristiano Ronaldo kwa Juventus kwa gharama ya pauni 99.2milioni.
Dirisha la usajili Italia litafungwa leo Ijumaa saa 3:00 Usiku.
Modric alijiunga na Real akitokea Tottenham mwaka 2012 amefanikiwa kutwaa taji moja la La Liga na makombe manne ya Ligi ya Mabingwa.
Inter imerejea katika Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2011-12.

No comments