Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

KOCHA MTIBWA AFUNGUKA NAMNA WALIVYOIRAHISISHIA SIMBA KUCHUKUA NGAO YA HISANI

Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amefunguka na kuweka hadharani sababu zilizowafanya Simba kupata ushindi na hatimaye kuchu...


Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amefunguka na kuweka hadharani sababu zilizowafanya Simba kupata ushindi na hatimaye kuchukua Ngao ya Hisani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jana.

Katwila amesema mabeki wa timu yake walikosa umakini ambao umesababisha Simba kutumia nafasi hizo kuwafunga mabao 2-1 na kuweza kuchukua taji hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Kocha huyo amesema Simba walifanikiwa kupata bao la kwanza ambalo Meddie Kagere alitupia kambani kutokana na beki wake kushindwa kuonesha utulivu kisha kuzidiwa ujanja na straika huyo ambaye alipasia kambani kiulaini.

Aidha, Katwila ameeleza kuwa bao la pili ambalo Simba walipata kupitia kwa Hassan Dilunga ambaye alisajiliwa kutoka kwao baada ya kung'ara msimu uliopita ulikuwa ni mpira wa kurushwa na mabeki walishindwa kuutuliza kisha kumpa nafasi mchezaji huyo kupiga shuti laini ambali kipa Benedict Tinocco alipishana nalo.

Mtibwa walikutana na Simba kwenye mchezo huo baada ya kutwaa ubingwa wa FA huku Simba wakibeba taji la Ligi 

No comments