Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Uhusiano wa Paul Pogba na United wazidi kupasuka

Siku ya leo magazeti mengi ya nchini Uingereza yameibuka na taarifa kwamba Paul Pogba anataka kuondoka na hajali nini kitatokea ila yuko t...



Siku ya leo magazeti mengi ya nchini Uingereza yameibuka na taarifa kwamba Paul Pogba anataka kuondoka na hajali nini kitatokea ila yuko tayari kulazimisha uhamisho huo utokee.


Pogba haswa amekuwa akiota kuichezea Barcelona na taarifa zinasema kwamba hata kwenda United haikuwa matakwa yake makuu, bali alitamani tangu mwanzo kwenda Barcelona au Real Madrid.
Katika mchezo wa kwanza wa United katika EPL hapo majuzi dhidi ya Leicester Paul Pogba alipewa kitambaa cha unahodha ili kujaribu kumshawishi kuendelea kuitumikia United.
Lakini baada ya mechi hiyo kuisha Pogba alinukuliwa akisema hawezi kuongelea nini mustakabali wake United kwani lolote atakalosema anaweza kupigwa faini.
Inadaiwa kwamba baada ya Pogba kutoa kauli hiyo, kocha Jose Mourinho amekasirika sana na kushtushwa na maneno ya Pogba na Ijumaa wiki hii anaweza kuongelea hali ya Pogba na United kwa sasa.
Mourinho ndio sababu kubwa ya Pogba kutaka kuondoka.
Kuna muunganiko wa sababu nyingi zinazotaka kumuondoa Paul Pogba Manchester United lakini sababu kubwa zaidi ni kocha wa Manchester United Jose Mourinho
Mourinho amekuwa akivutana na Pogba kuanzia uwanjani ambapo Paul huwa hafurahishwi na mbinu za Jose Mourinho ndani ya uwanja haswa za kujilinda na anatamani acheze kama alivyokuwa akicheza Juventus.
Kulikuwa na tetesi kwamba Pogba ameshawaambia baadhi ya wachezaji wenzake kwamba dili lake na Barcelona liko poa na anatamani likamilike aanze kwenda kuitumikia klabu hiyo.

No comments