Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

ZAHERA HANA HOFU NA WAARABU

Zahera hana hofu hata chembe na safu yake ya ulinzi ambayo inaongozwa na beki mkongwe, Kelvin Yondani ambaye hivi karibuni alipewa...











Zahera hana hofu hata chembe na safu yake ya ulinzi ambayo inaongozwa na beki mkongwe, Kelvin Yondani ambaye hivi karibuni alipewa unahodha wa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu wengine ni Andrew Vicent ‘Dante’, Juma Makapu na Juma Shaibu ‘Ninja’.

“Ninajisikia furaha kuona mabadiliko makubwa katika timu yangu kwa kuanzia safu yangu ya ulinzi niliyoitengeneza katika kipindi cha maandalizi tukiwa kambini kwa kuonyesha kiwango kikubwa ambacho kimenipa matumaini ya kufanya vema katika ligi na michuano mengine tutakayoshiriki.

“Nimefarijika baada ya mabeki wangu kucheza mechi tatu mfululizo za kirafiki bila ya kuruhusu bao, hicho ndiyo kitu nilichokuwa ninataka kukiona, kwani msingi wa timu unaanzia nyuma golini kwetu.

“Nimemuona Dante akiwa na fiziki ya kutosha katika mechi hizi tulizocheza kwa maana si yule niliyemkuta baada ya kumtengeneza vizuri katika fitinesi,” alisema Zahera ambaye makazi yake yapo karibu na Ufukwe wa Bahari ya Hindi maeneo ya Kawe

No comments