Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

SALAMBA AWEKA REKODI YA AINA YAKE TAIFA

Kama utani vile lakini maajabu yametokea Uwanja wa Taifa jana kwa aliyekuwa straika hatari wa Lipuli FC na sasa Simba, Adam Salamba kuchez...


Kama utani vile lakini maajabu yametokea Uwanja wa Taifa jana kwa aliyekuwa straika hatari wa Lipuli FC na sasa Simba, Adam Salamba kucheza takribani dakika 6 bila kufanya maajabu.

Salamba ambaye bado anaaminiwa kufanya makubwa ndani ya wekundu hao wa Msimbazi endapo akipunguza ubishoo, aliingia Uwanjani kipindi cha pili akichukua nafasi ya Nahodha, John Bocco wakati timu yake ikicheza na Tanzania Prisons.

Mchezaji huyo alishindwa kuonesha makeke yake Uwanjani na hii ilikuwa na kutokana na ukomavu wa beki ya Prisons ambayo iliwapa tabu Simba ya kuweza kutikisa nyavu zao.

Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa mapema kabisa na Meddie Kagere mnamo dakika ya pili tu ya mchezo aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC.

Baada ya Simba kuanza vema kwa ushindi kiduchu jana, watani zao wa jadi Yanga, leo wanashuka dimbani kuwakaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja huohuo wa Taifa.

No comments