Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

TANZANIA PRISONS WAWATISHA SIMBA

Wakati Simba wakitamba kuanza na ushindi katika harakati za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara leo, uongozi wa klabu ya Tanzania Prisons u...



Wakati Simba wakitamba kuanza na ushindi katika harakati za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara leo, uongozi wa klabu ya Tanzania Prisons umewataka wajiandae haswaa.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Prisons, Anvintishi Abdallah, amesema kuwa wao wameshajiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo utaokuwa wa kwanza kwao msimu hu.

Abdallah amewaahidi Simba kujiandaa vema kwani watakuja na moto wenye balaa la aina yake na ikiwezekana alama tatu zikaelekea jijini Mbeya.

Tayati Prisons walishawasili jijini Dar es Salaam wakiwa na siku kadhaa kwa ajili ya kipute hicho kitakachopigwa majira ya saa 1 kwenye Uwanja wa Taifa.


Wakati Simba wakianza kukupiga na Prisons leo, watani zao wa jadi wataanz mbio hizo za ubingwa kesho kwenye Uwanja huohuo kuwakaribisha Mtibwa Sugar FC ya Morogoro

No comments