Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

“Bado nipo, sitaondoka mwaka huu,”

CHELSEA imeshusha presha baada ya supastaa wake, Eden Hazard kuweka bayana ataendelea kuwepo klabuni hapo msimu huu. Hata hivyo,...

Image result for hazard chelsea sarri
CHELSEA imeshusha presha baada ya supastaa wake, Eden Hazard kuweka bayana ataendelea kuwepo klabuni hapo msimu huu.
Hata hivyo, nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji amegoma kuelezea hatima yake kama ataendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi ama ataondoka mwishoni mwa msimu.
Kwa muda mrefu sasa Hazard amekuwa akiwindwa na Real Madrid na mwenyewe mara kadhaa ameeleza nia yake ya kukipiga na mabingwa hao wa Ulaya.
Mabosi wa Chelsea walikuwa katika wakati mgumu wakiamini staa huyo angeondoka kwenye dirisha hili la usajili.
Juzi Jumamosi, Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri aliweka bayana kuwa Hazard hatauzwa kwa Real Madrid hadi pale atakapopatikana mrithi wake.
“Bado nipo, sitaondoka mwaka huu,” alisema Hazard ambaye juzi Jumamosi alitokea benchi na kutengeneza bao la ushindi kwa beki Marcos Alonso dhidi ya Arsenal.
Licha ya dirisha la usajili kwa England kufungwa, lakini Hazard, 27, bado alikuwa akihusishwa kuondoka kwenye dirisha hili kutokana na dirisha la Hispania kuendelea kuwa wazi hadi mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Hazard alisema: “Kila mmoja anafahamu kitu gani nilisema baada ya Kombe la Dunia, lakini nina furaha kuwepo hapa.
“Sipendi kuzungumza hili kabisa kwani, mengi yamesemwa ila kwa sasa nina furaha. Nina miaka miwili imebaki kwenye mkataba wangu, hivyo tutaona kitu gani kitatokea. Lakini, kuondoka mwaka huu, hapana sitaondoka.”
Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo Hispania na kutua Juventus kulionekana kumfungua milango Hazard kwenda Real Madrid huku supastaa wa Kibrazil na PSG, Neymar naye akipewa nafasi ya kujiunga na miamba hiyo ya La Liga.
Hata hivyo, imeelezwa Madrid haikuonyesha nia ya dhati kutaka saini ya Hazard na badala yake ilielekeza nguvu kumnasa kipa namba moja wa Chelsea, Thibaut Courtois.

No comments