Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

MCHEZAJI YANGA AWAPA WAKATI MGUMU SIMBA MSIMU UJAO

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Abeid Mziba, amesema uhakika wa Simba kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao upo shakani. Mche...


Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Abeid Mziba, amesema uhakika wa Simba kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao upo shakani.

Mchezaji huyo aliyewahi kutamba katika soka la Tanzania miaka ya 1980 mpaka 1990 amesema kutokana kurejea kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuph Manji anaamini klabu itakaa sawa na kuonesha upinzani mkali.

Yanga imekuwa ikipitia kipindi cha mpito tangu Manji atangaze kuachia ngazi hiyo takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita.

Mbali na ujio wa Manji, Mziba ameeleza namna Kocha wake, Mwinyi Zahera alivyokinoa kikosi na usajili mpya wa baadhi ya wachezaji utaamsha ari na kuleta ushindani kwenye ligi.

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa kundi D uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments