Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

“Hivi unaweza kumwambia Messi au Maradona arudi nyuma kukaba?”

KIWANGO cha kiungo wa fundi wa Kijerumani, Mesut Ozil kimezidi kuwavuruga wengi na sasa supastaa wa zamani wa Arsenal, Nwanko Kanu ameji...

Image result for ozil arsenal 2018
KIWANGO cha kiungo wa fundi wa Kijerumani, Mesut Ozil kimezidi kuwavuruga wengi na sasa supastaa wa zamani wa Arsenal, Nwanko Kanu amejivisha mabomu na kuingilia kati.
Kanu, ambaye amekuwa kimya huku Ozil akiendelea kukosolewa akidaiwa kucheza chini ya kiwango hasa kwenye mechi kubwa, sasa ameamua kimwaga ugali.
Mpachika mabao huyo aliyecheza kwa mafanikio Arsenal, amewataka mabosi wa klabu yake hiyo kuamua moja kumuacha Ozil acheze mpira wake ama wamuweka sokoni.

“Hivi unaweza kumwambia Messi au Maradona arudi nyuma kukaba?” Alihoji Kanu.
Kwa mujibu wa Kanu, amewataka Arsenal kukubaliana na staili ya uchezaji wa Ozil kwa kuwa hawezi kubadilika na wakiona ni tatizo zaidi basi wamuuze.
Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa klabuni Arsenal akipokea Pauni 300,000 kwa wiki na hilo limekuwa likimfanya kuwa kwenye matatizo kila timu inapopoteza mchezo.
Hata hivyo, Kocha wa Arsenal Unai Emery, amekuwa akijaribu kuzungumza na Ozil na kumtaka kutimiza majukumu yake uwanjani ili kusaidia timu kupata matokeo bora.
Lakini Kanu amemshauri Emery kumpa Ozil majukumu ya kuchezesha timu zaidi kwa kuwa, ndio eneo analolidumu zaidi na hapo ataona matokeo.

No comments