Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

RAGE AIBUKA NA TAMKO ZITO KWA VIONGOZI SIMBA

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amewataka viongozi wa klabu hiyo kutotetereka juu ya viongozi wake baadhi kuitwa kwe...


Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amewataka viongozi wa klabu hiyo kutotetereka juu ya viongozi wake baadhi kuitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Rage amewaomba Simba kuwatetea viongozi hao ambao ni Meneja wa timu, Richard Robert pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Robert Kisiwa baada ya kuitwa TFF kujibu suala la kusababisha wachezaji wa timu yao kuchelewa kuripoti kambini.

Kiongozi huyo amesema Simba wanapaswa kuwaunga mkono kwa kuwapa sapoti ili waweze kuwa washindi akieleza kuwa hakuna kosa lolote ambalo walilifanya.

Rage amewatetea Robert na Kisiwa kutokana na imani yake juu ya taratibu za kuwasili kwa wachezaji ndani ya timu ya taifa kuwa TFF hawatambui vizuri sheria za FIFA.

Mbali na kueleza hayo, Rage pia amesema TFF pamoja na Kocha Emmanuel Amunike, wamewaonea wachezaji hao kwa kuwapa adhabu kubwa na badala yake akashauri vema wangepewa onyo

No comments