Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Arsenal yampoteza Stephy Mavididi

Mshambuliaji huyu mwenye miaka 20 ambaye anaichezea timu ya Taifa ya England chini ya miaka 21 na ile ya chini ya miaka 23, m...















Mshambuliaji huyu mwenye miaka 20 ambaye anaichezea timu ya Taifa ya England chini ya miaka 21 na ile ya chini ya miaka 23, msimu uliopita alikuwa akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Charlton

Milan, Italia. Kwa mara nyingine klabu ya Arsenal imempoteza kinda wake Stephy Mavididi, ambaye anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitano Juventus.
Mshambuliaji huyu mwenye miaka 20 ambaye anaichezea timu ya Taifa ya England chini ya miaka 21 na ile ya chini ya miaka 23, msimu uliopita alikuwa akicheza kwa mkopo kwenye klabu ya Charlton.
Klabu ya Juventus imethibitisha kuwa imeafikiana kila kitu kuhusu maslahi binafasi na kinda huyo na kwamba amefuzu vipimo vya afya.
Mavididi, alijiunga na Arsenal kama mchezaji chipukizi na akasainishwa kuwa mchezaji wa kulipwa Julai, 2015.
Kuondoka kwa mchezaji huyo ni muendelezo wa Arsenal kuwapika wachezaji vijana na baadaye kutowathimini kiasi kwamba wengine huwaachia wakaondoka bila malipo na baadaye kuwarudisha kwa gharama kubwa.



No comments