Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

AKILIMALI ATOA TAMKO LAKE BAADA YA MANJI KUWASILI TAIFA JANA

Baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga kuwasili Uwanja wa Taifa kuishuhudia timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya U...


Baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga kuwasili Uwanja wa Taifa kuishuhudia timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali amesema hana tatizo naye.

Akilimali ameeleza kuwa anamtambua Manji kama Mwanachama na si Mwenyekiti wa klabu kutokana na kutangaza kuachia ngazi takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa mpaka sasa.

Mzee huyo amesema endapo akimsikia Manji kuwa ametangaza kurejea kwenye nafasi yake kwake hakuna tatizo na atampokea kwa mikoni miwili.

"Mimi sina shida na Manji, najua ameenda Uwanjani kama Mwanachama wa Yanga, endapo akisema anarudi kwenye nafasi yake, mimi sina shida kabisa, namkaribisha" alisema.

Ikumbukwe Maji alitangaza kuachia wadhifa huo kwa sababu alizozieleza kuwa anahitaji muda wa kupumzika pamoja na kufanya masuala yake mengine ya kibiashara

No comments