Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Singida United inajuta kuwafahamu nyota wa kigeni

Singida United imesema wamejifunza kwa makosa na hawatarudia tena kufanya usajili wa pupa kwa wachezaji wa kigeni. Meneja wa Singida Uni...


Singida United imesema wamejifunza kwa makosa na hawatarudia tena kufanya usajili wa pupa kwa wachezaji wa kigeni.
Meneja wa Singida United, Ibrahim Mohammed alisema walikuwa wakifanya usajili kwa mihemko bila kuwaona au kuwafuatilia vya kutosha wachezaji wa kigeni.
Alisema wametumia nyota wengi wa kigeni kwa msimu mmoja tu ambao walikuwa katika ligi lakini kosa hilo la kusajili bila kuzingatia vigezo walijikuta wachezaji hao hawana msaada na klabu.
"Tulikosea aina hiyo ya usajili tuliokuwa tunafanya, lakini msimu huu tumewapunguza wachezaji wengi wa kigeni na tumebaki nao watano tu tunaimani watafanya kile ambacho tunategemea kutoka kwao," alisema.
"Nyota wa kigeni wote ambao tumewasajili msimu huu tulikutana na benchi lote la ufundi, tuliwafuatilia vilivyo wachezaji wote tumewasajili na katika kuhakikisha kama hatujakosea wataonekana katika ligi," alisema Mohammed.

No comments