Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Okwi, Wawa wafunika mapokezi ya Simba

Mwanza.  Nyota wa Simba, Paschal Wawa na Emmanuel Okwi wamekuwa kivutio zaidi kwa mashabiki wa klabu hiyo Jijini hapa wa...









Mwanza. Nyota wa Simba, Paschal Wawa na Emmanuel Okwi wamekuwa kivutio zaidi kwa mashabiki wa klabu hiyo Jijini hapa walipowasili asubuhi kwa ndege ya Dreamliner kwa ajili ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar kesho.
Wachezaji Jonas Mkude, Mohammed Ibrahim, Marcel Kaheza na Said Ndemla walitangulia kutoka nje na kushangiliwa na zilizpopita takribani dakika tano nyota wengine walifuata, lakini alipotokezea Okwi kisha Wawa palilipuka shangwe, huku wakitajwa majina mara kadhaa.
Mashabiki hao walifurika katika mapokezi ya Wekundu hao, walitamani kuwashika mikono na kupiga picha nao, lakini mabaunsa waliweka ngumu kwa yeyote kutoruhusiwa kuwagusa.
Licha ya kuzuiwa kuwagusa, wapo ambao walifanikiwa kuwashika nguo.
Simba imetua jijini hapa majira ya saa 3:48 asubuhi na jioni ya leo wanatarajia kujifua kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya mchezo wao wa kesho.

No comments